Sunday, August 25

“Sikuwa kimya ila haukuwa wakati wangu”:- Recho

0


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania Recho Kizunguzungu anaamini kuwa kipindi alichokuwa hasikiki kwenye Muziki haukuwa muda sahihi kwake hivyo alikuwa akisubiri wakati ufike ndipo asikike tena.

Akipiga story na Dizzim Online msanii huyo ambae tayari ameachia wimbo wa ‘sameboy’ alishirikiana na Linah amesema sasa ni muda sahihi wa Mashabiki wake kuendelea kupata burudani nzuri kutoka kwake.

“Wakati  nipo kimya na wengine wanafanya kazi nilikuwa naona ndio wakati wao yani nafasi yao kwa kipindi kile na nilifurahi pia kwasababu hakukuwa na wasanii wengi wakike kwa kipindi kile so niliona wamezidi kusaidia” Amesema Recho.

Recho amewaomba mashabiki zake wakae mkao wa kula kwasababu siku si nyingi ataachia ngoma yake.

 

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.