Sunday, August 18

“Kufungia Nyimbo ni kutafuta kiki tu”- Belle9

0


Msanii wa muziki wa RnB kutoka Tanzania Damian Abelnego a.k.a Belle9, amesema suala la wasanii kufungiwa nyimbo zao na BASATA kwa upande wake haoni kama kuna lingie kubwa zaidi ya kiki tu.

Akizungumza na Dizzim Online Belle9 Amesema. mwanzoni alichukulia jambo hilo kuwa kubwa sana lakini kwasasa anaona ni mipango tu imepangwa na Watu fulani ili baadae wajipatie umaarufu na pongezi.

“Nimefanya reseach zangu jinsi watu wanavyo ongelea nimekuja kuona ni kiki tu basi yani suala fulani hivi ambalo limeanzishwa kupewa kiki watu fulani waongelewe alafu baadae anakuja mtu anasema anaamua ngoma ziachiwe alafu credit ziwe zake” Amesema Belle9.

Aidha msanii huyo amewaomba Watanzania wapiganie maendeleo yao waachane na mambo hayo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.