Wednesday, July 17

NAOMBA MSOME HAPA NA TUMPE USHAURI MAMA HAPA YUPO NJIA PANDA.

0


dina naomba uniombee ushauri wangu kwa wanawake wote na wanaume wanaopita ndani ya hii blog yako.mimi ni mfanyakazi mama wa watoto watatu wakike mmoja nilimzaa kabla ya kuolewa na hawa wawili ni mapacha wa kike jumla watatu. Mume wangu nilimkuta na mtoto mmoja wa kiume tatizo lililopo mtoto wangu mkubwa juzi kaniambia mama kaka ananivua chupi ananifanya mchezo mchafu tena sio mara moja kama mara mbili nikasema sawa subiri baba arudi. Baba alivyorudi tukakaa tukaongea akasema atafanyia uchunguzi swala hilo atatoa jibu. kwa kweli niliumia nikasema sawa saa ya kulala akaniambia wewe kama mama ulikuwa wapi mpaka mtoto anafanya hicho kitendo na umeshindwaje kumgundua kama ameanza mahusiano na kwanini asiseme toka siku ya kwanza anafanyiwa hicho kitendo nikawa nimechoka nilichofanya nikakaa kimya nafikiria kuachana na huyu bwana kwa ajili ya mwanangu nateseka moyoni jamani nipo kazini akili inawaza mwanangu alivyotendwa nifanyaje mimi na baba hanipi ushirikiano zaidi ananituhumu kweli hii??

  USHAURI WAKO PLS??Read More

Share.

About Author

Leave A Reply