Monday, August 19

Wambura aitwa kujua mbivu na mbichi

0


Kamati ya rufaa ya maadili ya shirikiso la soka Tanzania TFF imetangaza kukutana Jumamosi kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo Michael Wambura aliyefungiwa maisha kujishughulisha na masuala ya soka.

Kaimu afisa habari wa TFF Clifford ndimbo amethibitisha kuhusiana na taarifa hiyo.

“Kamati ya rufdaa ya maadili inataraji kukaa Jumamosi ya Machi 31 ambapo itakuwa saa 5 asubuhi, pamoja na mambo mengine pia itasikiliza rufaa ya Michael Wambura ambaye alikata rufaa.”

“Anaruhusiwa kuja kutoa utetezi wake kwa njia ya mdomo, maandishi au kuleta vielelezo vyote vya utetezi wake pia anaweza kuleta mwakilishi akiwa na barua ya uwakilishi au anaweza kuamua kutokuja kabisa.”

“Tayari wito wake ameshapelekewa na bila shaka atakuwa amesha upokea, kuelekea katika shauri hilo siku ya Jumamosi gharama zitakuwa juu yake mwenyewe.”

Wakili wa Wambura Emanuel Muga amesema mteja wake amepokea wito kutoka kamati ya rufaa ya maadili na atakwenda kutetea haki yake mbele ya kamati hiyo.

“Ni kweli Michael Wambura amenieleza kwamba amepata wito na wito huo ni kwa ajili ya kikao cha Machi 31 saa 5 asubuhi pale TFF atakapoenda kusikilizwa.”

“Wambura amesema yupo tayari kwenda kutetea haki yake mbele ya kamati na ana hoja zake na amethibitisha kwamba atakwenda.”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.