Tuesday, May 21

Viwanja Tanzania kukaguliwa

0

Ujumbe wa shirikisho la soka Afrika (CAF) unatarajiwa kutua nchini December 15 kwa ajili ya kutembelea na kukagua maandalizi uenyeji wa fainali za AFCON U17 2019.

“December 15 au 16 wanaingia viongozi wa Caf kwa ajili ya ukaguzi wa miundombinu na December 20 kuna draw, ni kitu kikubwa sana katika mpira kwa hiyo macho yote duniani yataelekezwa Tanzania wakati tunafanya draw ya mashindano AFCON ya mwakani”-Dr. Harrison Mwakyembe, Waziri mwenye dhamana ya michezo.”

“Sisi tunajiandaa kwa sababu wanakuja kukagua kama kweli tumepiga hatua nashukuru mabadiliko makubwa yamefanyika Chamazi, mabadiliko makubwa yanafanyika uwanja wa taifa, uwanja wa Uhuru tayari tumeshaagiza carpet. Nafikiri kufikia mwezi January uwanja wa Uhuru utakuwa umebadilika.”

“Kufikia mwezi March tutakuwa tumeshamaliza kabisa uwanja wa Uhuru, pesa inahitajika zaidi, tutahangaika tutafanya barambee lakini lazima uwanja wa Uhuru uwe tayari kufikia mwezi wa tatu ili utumike mwezi wa nne kama kiwanja cha mazoezi.”

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply