Sunday, August 25

Video-Himid Mao na Hemed Morocco wamezunguza kuelekea mechi ya Stars vs DR Congo

0


Timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya DR Congo mchezo ambao upo kwenye kalenda ya fifa. Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Jumanne ya Machi 27, 2018 uwanja wa taifa.

Mchezo huo unakuja baada ya taifa Stars kupoteza mechi yake ya kirafiki kwa kufungwa 4-1 ugenini dhidi ya Algeria Machi 22, 2018 uwanja wa Stade du 5 Juillet mjini Algiers.

Kuelekea mechi dhidi ya DR Congo, kocha msaidizi wa Stars Hemed Morocco pamoja na nahodha msaidizi Himid Mao wamezungumza na waandishi wa habari kuelezea maandalizi huku wachezaji Aishi Manula na Abdulazizi Makame wakiukosa mchezo huo kutokana na majeraha.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.