Sunday, August 25

TFF inapokosea tunasema, lakini kwa hili tuko pamoja”-Shaffih Dauda

0


Stars ipo jijini Algiers kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji Algeria leo Machi 22, 2018 na baada ya mchezo, itarejea nyumbani kucheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Congo DR Machi 27, 208 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchambuzi wa masuala ya michezo nchini bw. Shaffih dauda amevutiwa na mipango ya tff kuamua kutafuta timu ambazo zimeidi tanzania katika viwango vya soka vya fifa.

Dauda ameamua kuja na ule msemo kwamba, ‘mnyonge mnyongeni haki yake mpeni’ akiwa na maana kwamba, kwa muda mrefu kilio cha wadau wa soka ilikuwa ni kuona timu yao ya taifa ikicheza mechi za kirafiki na mataifa makubwa nay aliyoendelea na kupiga hatua zaidi afrika.

“Nimeipenda mipango ya TFF, lazima tuwapongeze katika hili kwa sababu tulikuwa tunawaponda walipokuwa wanatafuta mechi za kirafiki dhidi ya Malawi  mara wanarudiana na Burundi”-amesema Dauda.

“Wamekuwa wasikivu wametafuta timu zilizotuacha mbali kwenye viwango vya Fifa, Stars itacheza na Algeria baada ya hapo itakutana na Congo DR, unaona kabisa wapo kwenye mipango.”

“Unapocheza na Algeria na Congo DR na kupata matokeo dhidi yao ambao wako juu kwenye viwango vya Fifa maana yake utapata pointi nyingi ambazo zitakuwezesha kupanda zaidi kwenye viwango.”

“Kwa hiyo kwa hilo wamekuwa na mpango mzuri na tutashuhudia game nzuri kwa sababu ili ujipime lazima ucheze na timu kubwa zilizokuzidi.”

Mara ya mwisho stars kucheza mechi ya kirafiki nyumbani ilikuwa ni Oktoba 7, 2017 ilipotoka sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Malawi uwanja wa Uhuru ikacheza mchezo wake wa kirafiki ugenini Novemba 12 dhidi ya Benin na kutoka sare ya kufungana 1-1.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.