Wednesday, August 21

Taifa Stars inahitaji kocha wa kigeni? Samatta amejibu

0


Baada ya mchezo kumalizika, nahodha wa Tafa Stars Mbwana Samatta amezungumzia michezo miwili ya kirafiki ambayo wamefanikiwa kucheza dhidi ya timu ambazo zimeizidi Tanzania kwa viwango vya Fifa.

“Ni game ambazo kama Tanzania inazihitaji, game ngumu lakini mwisho wa siku kama hivi unavyopata matokeo unakuwa umejisogeza kiasi fulani katika viwango vya Fifa lakini usipopata matokeo vilevile inakuwa imekusaidia kukujengea kujiamini  na uzoefu.”

Samatta pia akasema njia rahisi ya kuifanya timu ya taifa iwe na mafanikio kwa muda mfupi au kuijenga kwa muda mfupi ni ni kuwa na professional wengi.

“Tunawahitaji wengi zaidi, wachezaji ni wazuri wana vipaji lakini kuna kitu fulani wanakipata wanapokuwa kwenye professional kwa hivyo tunahitaji tupate wengi zaidi. Njia rahisi ya kuifanya timu ya taifa iwe na matokeo kwa muda mfupi au kuijenga kwa muda mfupi tuwe na professional wengi wakati tunasubiri wadogo zetu wakiwa wanachipukia lakini kwa sasa pia tunahitaji matokeo kwa hiyo tukipata professional wengi watatusaidia.

Wakati tunazungumzia professional wengi, tayari kuna watu wameanza kusema kwamba tunahitaji kocha wa kigeni kwa ajili ya kuisogeza stars kutoka ilipo, Samatta alipoulizwa kama timu ya taifa inahitaji kocha wa kigeni alijibu: “No comment”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.