Thursday, August 22

“Stars kufungwa 4-1 Algeria ilikuwa mtaji”-Shaffih Dauda

0


Ushindi wa 2-0 iliopata timuya ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umerejesha faraja kwa watanzania baada ya siku chache kuiona timu yao ikipoteza mbele ya Algeria kwa kipigo kikali cha mabao 4-1.

Mchambuzi wa masuala ya michezo Shaffih Dauda amesema, Stars kufungwa 4-1 na Algeria ndio ulikuwa msingi wa ushindi dhidi ya DRC.

“Pamoja na kufungwa 4-1 na Algeria nimeona ndio ilikuwa msingi wa ushindi wa Stars dhidi ya DRC kwa sababu baada ya ile mechi walikuwa tofauti kwenye mechi dhidi ya Congo.”

“Walikuwa hawaogopi, walionekana wanataka matokeo na hicho ndio kitu ambacho huwa kina kosekana. Tangu mwanzo wa mchezo walionekana wanataka matokeo.”

Dauda pia amesema alifarijika alipoona ratiba ya mechi za kirafiki dhidi ya Algeria pamoja na DRC kwa sababu ni mataifa ambayo yapo juu kwenye soka la Afrika na yanawachezaji wengi wanaocheza Ulaya.

“Matokeo dhidi ya DRC ni mazuri sana kwa wachezaji wa Tanzania, yanawajengea kujiamini.”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.