Monday, March 18

Simba kukutana na Hassan Kessy kimataifa

0

Klabu ya Simba huenda ikakutana na Hassan Kessy hatua ya pili ya klabu bingwa Afrika 2018/19. Simba itakutana na mshindi kati ya Nkana FC ya Zambia (timu anayochezea Kessy) au UD Songo ya Msumbiji.

Leo Jumatano Dec 5, 2018 inachezwa mechi mechi ya marudiano Nkana FC vs UD Songo itakayoamua timu itakayokutana na Simba katika hatua ya pili.

Katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa Msumbiji, Nkana ilishinda 2-1 na Nkana ndio inapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele hatua inayofuata. Kama itakuwa hivyo Simba itakutana na mchezaji wake wa zamani Hassan Kessy.

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply