Tuesday, March 19

“Nipo Tayari kwa ligi kuu”-King Kiba

0

Ali Kiba ambaye ni mchezaji na mdhamini wa Coastal Union amesema yupo tayari kuitumikia klabu hiyo mara baada ya kumaliza majukumu yake ya kimuziki ndani na nje ya nchi. Kwa sasa anatekeleza program za mwalimu baada ya kukosekana kwenye timu kwa muda mrefu.

“Mpaka sasa hivi nipo tayari, kwa sababu nipo wiki nzima na tumeshazoeana na tunajua ni jinsi gani na mfumo gani tunacheza kwa hiyo siyo ngumu sana kwa mchezaji mzoefu kama mimi kwa sababu nipo kwenye mpira kwa muda mrefu nadhani kwa sasa nipo tayari.”

“Lengo siyo kung’aa, lengo ni kufanikisha ushindi, kwa sababu team work inamaanisha mchango wangu pia upo. Kung’aa ni tofauti na kucheza vizuri, lengo ni sisi kupata ushindi tu.”

Tangu Ali Kiba amesajiliwa na Coastal Union bado hajacheza mechi yoyote ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu.

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply