Sunday, August 18

Manara amekataa auzalendo wa kinafiki “Kila mtu afe kivyake”

0


Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kwa sasa hakuna sula la uzalendo kuiunga mkono Yanga ambayo itaendelea kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kutolewa kwenye kombe la vilabu bingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya magoli 2-1 na Township Rollers katika michezo miwili ya raundi ya kwanza.

Manara ambaye klabu ya Simba imetolewa na Al Masry kwa faida ya goli la ugenini baada ya sare ya 2-2 uwanja taifa kisha kutoka suluhu Misri, aliwahi kuwasihi mashabiki wa Simba kutoizomea Yanga wakati ikicheza mechi zake za kimataifa kwa sababu itakuwa ikiiwakisha nchi.

Lakini Manara alipingwa na baadhi ya viongozi wa Yanga wakisema hatoweza kuishangilia Simba, baada ya Yanga kuangukia michuano ya shirikisho Afrika, baadhi ya wadau wa timu hiyo wameomba watanzania kuwa wazalendo kwa kuiunga mkono kwa sababu ndiyo timu pekee ambayo inawakisha taifa kwa sasa jambo ambalo limepingwa kwa nguvu na Haji Manara.

“Mimi ndio nilitoa hoja ya uzalendo kabla ya kucheza na washelisheli na wadjibout, niliongea kama mtanzania nikiwa kiongozi wa klabu na nikawaambia wanachama wetu na mashabiki wetu wasiende kuizomea Yanga na kuwasihi watanzania tuwe na utamaduni huo.

Mimi nimesafiri dunia hii naifahamu, vituko vyetu tunavyofanya ni mara chache kuona kwenye viwanja vya ugenini. Tunachofanya sisi kwa lugha rahisi unaweza kusema ni ushamba na ulimbukeni, hakuna faida yoyote tunayopata kama nchi kwa mambo ya kijinga.

Baada ya  sisi kutolewa na Al Masry na Yanga kwamba wataendelea kucheza kombe la shirikisho, nimeona baadhi ya watu wa Yanga wanazungumza mitandaoni kuhusu suala la uzalendo, uzalendo huu ndio unakuja sasa hivi wakati mimi nilipingwa na hamkukosoa?

“Sasa hivi mimi nakataa sitaki uzalendo, uzalendo nitakaosimamia mimi ni kutangaza vivutio vya kitalii na vitu vingine itatosha lakini uzalendo sio lazima kuishangilia Yanga, mbona wao walikataa? Uzalendo huo uje sasa hivi, no way.”

“Wanasimba kataeni uzalendo kipindi hiki, sasa hivi shughulikeni na vivutio vya utalii, uzalendo feki sitaki kuusikia kwa sababu niliposema mimi Mkemi alinipinga na hakuna hata kiongozi mmoja wa Yanga alitoka kuikanusha wala kuipinga kauli ya Mkemi.”

“Wanasimba siku Yanga wakicheza mechi vaeni jezi ya hiyo timu maana ndio wanataka.”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.