Monday, August 19

Kwa mipango hii ya Township, Yanga acha watolewe tu

0


Wababe wa yanga katika kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la klabu bingwa afrika township rollers ya Botswana kumbe sio wa mchezo kabisa, walijipanga kwa ajili ya kufika walipo sasa katika soka la vilabu barani afrika.

Kufuzu kwao hatua ya makundi kwa kuiondosha yanga hakujaja kama ‘zali’ bali wamefanikiwa kutokana na mipango yao kabla hata hawajaanza kucheza mashindano hayo msimu huu.

Lyatile Mute ni mtangazaji wa kituo cha Duma FM radio nchini Botswana amefichua siri ya mafaniko ya timu hiyo ambayo imefuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

“Tangu mwaka jana walikuwa na ndoto ya kuliteka bara la Afrika kwa sababu waligundua kuwa wamefanikiwa sana nchini Botswana na sasa walitaka kusogea mbele zaidi.”

“Moja kati ya mipango yao walitaka kumwajiri kocha ambaye atawasaidia katika malengo yao na zaidi ya hapo walimwajiri mkurugenzi wa ufundi ambaye ana uzoefu mkubwa na kocha Nicola Kavazovic anatokea Serbia na mkurugenzi wa ufundi ambaye anajukumu la kufanya tathmini kuhusu michezo mbalimbali hasa ya wapinzani kabla ya mchezo na wakati wa mchezo.”

“Siku zote husafiri kufuatilia wapinzani na kuripoti kwa mwalimu, mkurugenzi wa ufundi wa Township ni mzuri katika kuzisoma timu pinzani kiufundi na namna ya kukabiliana na timu pinzani.”

“Wakati wa mechi hukaa eneo la VIP ambapo anawezeza kuona mechi na kuwasaidia wakati wa mapumziko na kumwambia mwalimu maeneo ya kuyafanyia kazi ili waweze kumdhibiti mpinzani.”

“Kingine kinachoisaidia Township ni uwepo wa teknolojia ya video ambayo inaweza kufanya tathmini nzuri kwa timu pinzani. Teknolojia ya video ni sehemu ya mipango ya timu kuwajua wapinzani na wamefanikiwa kwa sababu wakati wa mechi inakuwa rahisi kukabiliana na wapinzani na imekuwa na msaada sana.”

“Pia wameongeza watu katika eneo la utabibu ambapo kuna daktari wa timu, mtaalamu wa viungo, mtaalam wa saikolojia, na hivyo wana timu kubwa katika eneo la kitabibu karibia watu watano. Watu hawa wanajukumu kubwa ikiwemo kuhakikisha wanawasaidia wachezaji kupona haraka kutoka majeruhi yao.”

“Hizi ndio sababu Township imekuwa bora hata saikolojia ya timu kusonga mbele ni kwa mchezaji kufurahia mchezo na kufuzu hatua ya makundi. Yote hii pia ni kwa sababu ya falsafa ya timu, falsafa ya timu inafanana sana na ile ya Mamelodi Sundowns, hauzuii bali njia ya kujilinda ni kumiliki mpira na kushambulia.”

Kama unakumbuka, township kabla ya kukutana na yanga waliitoa al merreikh kwa kuifunga 3-0 wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kisha wakapoteza mchezo wa marudiano kwa kufungwa 2-1 na kufanikiwa kusonga mbele kwa aggregate ya 4-2.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.