Sunday, December 16

Kocha amkingia kifua Kindoki Yanga

0

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amewaambia baadhi ya mashabiki wa timu yake wafunge midomo yao, ni wale wanaomtupia lawama golikipa Klaus Kindoki baada ya kufungwa magoli mawili na Sumbawanga United kwenye mchezo wa kirafiki.

“Mashabiki wa Yanga wanaomlaumu Kindoki kufungwa magoli mawili dhidi ya Sumbawanga United wanyamaze kimya, hawajui mpira, wafunge midomo yao.”

“Beki ana mpira halafu uwanja mbaya, badala ya kupiga mpira anamsubiri mshambuliaji ampige chenga matokeo yake ananyang’anywa mpira tunafungwa, ni kosa la Kindoki?

“Magoli mawili tuliyofungwa Sumbawanga hakuna hata goli moja limetokana na Kindoki, golikipa yeyote duniani angefungwa. Sasa kosa la Kindoki liko wapi?

Chanzo @ufmradiotz

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply