Wednesday, August 21

Kamati ya rufaa ya maadili imetusikiliza vizuri, tunasubiri hukumu”-wakili wa Wambura

0


Kamati ya maadili ya rufaa imekutana leo Machi 31, 2018 kusikiliza rufaa ya aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ambaye alikata rufaa baada ya kamati ya maadili kumfungia maisha kujihusisha na soka.

Wakili wa Wambura Emanuel Muga amesema, kamati imewasikiliza vizuri chini ya mwenyekiti wake Ebeneza Mshana na kile walichotakiwa kukisema kimepokelewa.

“Kikao kimeisha tunasubiri kamati ifanye maamuzi, tumekwenda pale kuwasilisha au kutetea hoja  za rufaa ambazo zilikuwa tano, kikao kikakaa chini ya mwenyekiti Ebeneza Mshana kikatusikiliza kwa utulivu.”

“Hoja zote za upande wa Wambura zimesikilizwa na upande wa TFF ukasikilizwa, hivi sasa tunasubiri hukumu. Tunachokifanya sisi ni kuwasilisha hoja za kisheria ambazo tunadhani zina mantiki suala la maamuzi tunawaachia kamati.”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.