Sunday, August 18

Hatua alizochukua wakili wa Wambura baada ya rufaa kukwama TFF

0


Wakili Emanuel Muga anaemtetea aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameeleza hatua anazochukua baada ya Jumamosi kukwama kuwasilisha rufaa ya mteja wake.

“Ni kweli Jumamosi tulikwenda TFF kuwasilisha rufaa lakini tukakuta ofisi zimefungwa, tulipojaribu kuwasiliana na watu wa TFF wakasema wangekuja ili wapokee hiyo rufaa tukaondoka tukarudi mara mbili hakukuwa na utashi wa kupokea rufaa na siku zilikuwa zinaisha kwa sababu hukumu ikishatoka mkata rufaa anakuwa na siku tatu za kukata rufaa.”

“Kwa hiyo tukaona tusipoteze muda tukaona tutumie njia nyingine ya kupeleka rufaa ambayo ni njia ya posta (EMS) inatambulika na kanuni ni njia moja wapo ya kuwasilisha nyaraka kwa hiyo tukaenda posta tukaituma tukapewa risiti.”

“Ijumaa nilimtuma kijana kutoka ofisini kwangu kuwasilisha hiyo rufaa TFF, akafika saa 10:15 jioni wakamwambia sio muda wa kazi lakini aliwakuta watu wakakataa kupokea kwa madai haukuwa muda wa kazi na hawaruhusiwi kupokea hizo nyaraka.”

“Kimsingi siku tatu za kukata rufaa ni baada ya kukabidhiwa hati ya hukumu, unaweza kukata rufaa kabla au baada ya kupata hukumu lakini hizi kamati zinaamua bila kufuata utaratibu, unaweza ukasubiri hati ya hukumu siku tatu zikapita wakatafsiri cha kwao kwa hiyo hatukutaka kuwapa nafasi ya kutafsiri cha kwao.”

“Tumekata rufaa kwa hati ya dharura ili isikilizwe haraka ili aendelee kufanya majukumu yake ya kimataifa, kitaifa na kimkoa. Kwa sababu tungeomba nakala ya hukumu, ingechukua miezi sita kwa sababu kuna watu nawatetea TFF kama Joseph Kanakamfumu hukumu yake imetoka muda mrefu lakini nimeandika kuiomba nakala ya hukumu bado hawajanipa.”

Leo Jumatatu Machi 19, 2018 muga atapeleka rufaa ya wambura kwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya maadili wakili ebeneza mshana kwa sababu kanuni zinaruhusu. Muga anahofia kwamba huenda TFF ikachelewa kuita kamati ya rufaa ya maadili.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.