Tuesday, August 20

Goms United yasimamisha mabingwa Ndondo Super Cup

0


Goms United imefanikiwa kufuzu fainali ya Ndondo Super Cup baada ya kuifunga Itezi 3-2 katika mchezo  huo uliochezwa uwaja wa Bandari, Temeke, Dar es Salaam.

Misosi ni washindi wa pili wa Ndondo Cup 2017 Dar ambapo mabingwa wa taji hilo walikuwa Misosi huku Itezi wakiwa ndio mabingwa wa Ndondo Cup 2017 Mbeya.

Nahodha wa Itezi Romario Albert ameeleza sababu iliyopelekea timu yao kupoteza mcheo huo.

“Mechi ilikuwa nzuri tuliweza kutawala mchezo kwa dakika zote 90 lakini Mungu hakupenda, tumeshindwa kupata matokeo kwenye mchezo wetu. Wanambeya wasikate tamaa waziti kutu-support tunaweza kupambana tukachukua nafasi ya mshindi wa tatu”- Romario Albert.

Paul John amesema waliruhusu magoli mawili kipindi cha kwanza kutokana na kuidhauu timj ya Goms

“Tuliwadharau Itezi kwa sababu tjlikuwa tunacheza mpira kwa kuwaskilizia ndio maana kipindi cha kwanza walifanikiwa wakatufunga 2-1. Tulivyoingi vyumba vya kubadilishi kocha akatupa mbinu mpya za kutumia tukaongoza juhudi ndio maana tumepata matokeo.”

“Wapenzi wote wa Goms wakae mkao wa kula safari haturudii makosa kwa sababu mara kwanz tulitereza lakini safari hii tupo vizuri.”Read More

Share.

About Author

Comments are closed.