Saturday, August 17

Fainali Ndondo Cup 2017 yajirudia 2018

0


Ile fainali ya Ndondo Cup 2017 kati ya Misosi FC dhidi ya Goms United hatimaye inajirudia tena katika fainali ya Ndondo Super Cup 2018 baada ya Misosi FC kufuzu hatua hiyo kwa kuifunga 2-0 timu ya Mnadani kutoka Mwanza.

Manahodha wa timu zote mbili wamezungumzia matokeo baada ya mechi kumalizika.

“Nimeumizwa na matokeo ambayo tumepata, tumefungwa 2-0 matokeo si mazuri kwetu kwa sababu hakuna mtu anayependa kufungwa”-Meshack Bona, nahodha Mnadani FC.

“Hakuna walichotuzidi isipokuwa walitumia vizuri nafasi walizopata lakini sisi tulishindwa kutumia nafasi tulizopata.”

“Tunajipanga vizuri hatuwezi kukata tamaa kwa sababu tumepoteza mechi ya leo, tutarekebisha mapungufu yaliyopo na kuongeza juhudi ili tushinde mchezo wa kufafuta mshindi wa tatu.”

“Kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri kwakuwa tuliwadharau wapinzani wetu lakini tulivyoenda mapumziko tukakubaliana hii ni mechi kama zilivyo nyingine na hakuna sehemu ya kurekebisha makosa”-Emanuel Memba, nahodha Misosi FC.

Michuano ya Ndondo Super Cup ilianza jana Jumamosi Februari 17, 2018 kwenye uwanja wa Bandari-Temeke mchezo ulioshuhudiwa Goms United ikiuuzu fainali ya michuano hiyo kufuatia kufanikiwa kuifunga Itezi  United 3-2.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.