Friday, August 23

Barua ya Kiemba kwa mashabiki baada ya kustaafu

0


Machi 24, 2018 Amri Kiemba na Thomas Maurice wameingia kwenye vitabu vya historia vya soka la Tanzania baada ya kutangaza rasmi kustaafu soka la ushindani kwa heshima kwa kucheza mchezo maalum uliojumuisha mastaa  mbalimbali wa zamani hata wa sasa.

Baada ya kutundika daruga, Kiemba ameandika barua kwa mashabiki kuwashuruku kwa kumuunga mkono katika kipindi chote cha uchezaji hadi alipoamua kustaau kwa hiari.

Napenda kuwashukuru ndugu jamaa na marafiki kwa upendo wenu mlionionyesha kwa kipindi chote nilichokua nikicheza soka nilipo anguka hamkuniacha mlijaribu kuniinua najua mimi kama mwanadamu nimekua nikiwakwaza kwa namna moja ama nyingine asanteni kwa kunivumilia mpaka napokuja kuwaaga na kuachana na soka la ushindani.

Pia niwashukuru wale waliokua wakitafuta mapungufu yangu na kuyatangaza hadharani sababu hao ndio nimekua nikiwatumia kama kioo cha kujitazamia na kujua wapi hapaendi vizuri sababu wale wanao kupenda huwa hawana muda wa kujihangaisha kuyatazama mabaya au hata kusikia yakielezewa niwashukuru kwa dhati waliokua wakinikosoa kwa namna moja ama nyingine iwe ni uchezaji wangu au aina yangu ya maisha ni wahakikishie sijawahi kuwachukia wala hamjawahi kuwa maadui kwangu nawapenda na ninawahitaji saana kwenye safari yangu ya maisha iliyobakia.

Niwashukuru kwa dhati waandishi wa habari kwa mchango wao kwangu kunifanya kuwa mimi naamini bila vyombo vya habari sijui kama leo ningekua wa namna nilivyo siwezi kusema ni maarufu ila najulikana.

Wapenzi wa soka nao nawashukuru kwa ushirikiano wao bila kujali itikadi zao za timu sababu nimekua nikipata ushirikiano wa kutosha kwa timu zote nilizofanya nazo kazi.

Naishukuru familia yangu kwa kunipa ushirikiano namshukuru mama yangu na kumpa pole kwa maumivu aliyokuwa akiyapata kila ninapopata misukosuko kwenye vilabu vyetu.

Siwezi kumsahau mke wangu kwani naye amehusika sana kunifanya mimi kuwa hivi nilivyo leo nikisema amehusika najua wale wenye wake kama mimi wananielewa kwa sababu kama hakuna maelewano au nyumba haina furaha sidhani kama ningefanya kazi yangu kwa ufasaha, NAKUPENDA SANA MKE WANGU na pole kwa misukosuko ya maisha ya kujulikana.

Watoto wangu wamekua ni washabiki wangu wakubwa na wao kwao hakuna mchezaji mzuri kuliko baba yao nawashukuru kwani pia nilikua naogopa kuwaangusha kwa kujitahidi kufanya vizuri.

Siwezi kuwamaliza wote sababu walionifikisha hapa ni wengi ila nawataja wachache kuonesha kwamba nathamini yote mlio nitendea.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nitamsahau mzee wangu Iddi Omari Kipingu, simzungumzii sana kwa sababu anajua ni kiasi gani nathamini alichofanya kwenye safari yangu ki soka.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.