Monday, August 19

Azam yabaki njia moja kimataifa

0


Mtibwa Sugar imeiondosha Azam kwenye michuano ya kombe la shirikisho Tanzania bara ‘Azam Sports Federation Cup’ kwa mikwaju ya penati 9-8 baada ya timu hizo kutoka suluhu ndani ya dakika 90.

Azam ambayo ilishiriki michuano ya kimataifa msimu uliopita inabidi ishinde taji la ligi kuu Tanzania bara ili kuweza kucheza mashindano ya Afrika msimu ujao.

Ipo nafasi ya nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 22 nyuma ya Yanga na Simba ambazo zina pointi 46 huku Yanga ikiwa imecheza mechi 21 wakati Simba yenyewe imecheza michezo 20.

Mibwa Sugar inaungana na Stand United na JKT Tanzania ambazo zimeshafuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambayo bingwa anaiwakilisha Tanzania bara kwenye mashindano ya kombe la shirikisho Afrika.

Jumapili Aprili 1, 2018 utachezwa mchezo mwingine wa robo fainali ya ASFC kati ya Singida United na Yanga ambapo mshindi atakamilisha idadi ya timu nne zitakazocheza hatua ya nusu fainali.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.