Saturday, August 24

Ammy Ninje anaamini Ngorongoro itapata ushindi mkubwa ugenini

0


Timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ imeshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya kikosi cha DR Congo kufuatia kulazimishwa suluhu katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa vijana wa U20.

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje amesema licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kupata magoli, walizidiwa nguvu na wapinzani wao.

“Tumejaribu kutengeneza nafasi nyingi kipindi cha kwanza lakini hatukupata goli na mpira ndiyo upo hivyo, ukiangalia wenzetu kwenye walikuwa vizuri katika kutumia nguvu kwa hiyo itabidi nije na mbinu nyingine kwenye mchezo wa ugenini tujue tutachezaje kwa kutumia nguvu vilevile kutumia nafasi kufunga.”

“Kiujumla wachezaji wamecheza vizuri kwa maelekezo waliyopewa lakini tuliona kulikuwa na penati moja au mbili bahati mbaya hatukupata. Mimi nadhani ushindi mkubwa tutapata kwao kwa sababu watafunguka kutaka kushambulia ambayo ndiyo mazoea ya timu nyingi zinapocheza nyumbani zinataka kufunguka.”

Ngorongoro Heroes itacheza mchezo wa marudiano na DR Congo siku tano baadaye jijini Kinshasa, mshindi wa mchezo huo (Tanzania vs DR Congo atacheza dhidi ya Mali katika raundi ya pili itakayochezwa mwezi Mei mwaka huu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.