Tuesday, March 19

Ambokile kuhusu kwenda Yanga, Simba

0


Akiwa uwanjani hutumia nguvu, kasi na akili, ukitazama kwenye orodha ya wafungaji wa ligi kuu Tanzania bara hadi sasa yeye ndio kinara wa kuzipasia nyavu akiwa ameshafunga magoli tisa (9) namzungumzia mshambuliaji wa Mbeya City Eliud David Ambokile.

Msimu uliopita alimaliza akiwa na mabao 10, nini kinamfanya Ambokile awe bora?

“Kikubwa ni kujitambua, kujituma na kusikiliza maelekezo ya wenzako na maelekezo ya mwalimu. Kingine kinachonifanya nionekane bora ni kutokana na timu yangu tunavyopeana ushirikiano kuanzia wachezaji benchi la ufundi na uongozi.”

Anafanya nini anapokuwa nje ya uwanja

“Napenda sana kushinda nyumbani kupiga story na wadogozangu, dadaangu pamoja na mzee wangu kwa sababu ndio watu ambao nipo nao kwa muda mwingi.”

“Mimi sio mtu mwenye mizunguko mingi, nikitoka mazoezini nalala na kupumzika. Ninapokuwa nyumbani napenda kuangalia mpira narudia kuangalia mechi ambazo nilicheza na mechi za ligi za nje England na Spain ambazo naweza kujifunza.”

Ukweli upoje kuhusu kuhusishwa na Simba na Yanga

“Bado sijapata ofa kwa sababu bado nina mkataba na timu yangu, kikubwa najua kama kuna lolote basi watazungumza na uongozi wa timu yangu wakamalizana lakini mimi popote nacheza kwa sababu ni mchezaji na ndio kazi yangu.”

Ambokile ni mpenzi na shabiki wa muziki

“Wanamuziki wengi nawasikiliza lakini namkubali sana Ali Kiba, kwa muda mrefu sasa nimekuwa nasikiliza nyimbo zake. Kuna wimbo unaitwa Mali Yangu ambao upo hadi kwenye simu yangu ni wimbo mzuri ambao hata hapa nyumbani watu huwa wanausikiliza.”

Ushauri kutoka kwa dada yake Ambokile (Joyce Ambokile)

“Ambokile ni mdogoangu wa tatu, namshauri aendelee kuwa na nidhamu, bila nidhamu hawezi kufika mbele. Amheshimu kila mtu asiwe na dharau.”

Comments

comments

Share.

About Author

Leave A Reply