Monday, August 19

Aliyewaleta kwenye soka ndiye aliyewastaafisha Kiemba, Maurice

0


Kanali mstaafu Idd Kipingu alikuwa mgeni rasmi wa mchezo wa heshima wa kuwaaga Amri Kiemba na Thomas Maurice, Kipingu aliwahi kuwafundisha wote wawili katika shule ya Makongo na leo alikuwa akiwashuhudia wanastaafu soka.

“Leo ni siku nzuri watoto wetu wanatamka rasmi kwamba wanaachana na soka la ushindani na hatimaye umati mkubwa umejikusanya kwa ajili hiyo, nawashukuru nawapongeza.”

“Nawashukuru wote waliojitokeza kuwapa heshima vijana wetu, kila anaeingia kwa hodi lazima atoke kwa kwaheri.”

Kipingu amesema alimtoa Tanga Amri Kiemba kwenye mashindano ya UMISETA na kumpeleka shule ya Makongo mwishoni mwa miaka ya 90 lakini Thomas Maurice alijiunga kidato cha kwanza katika shule hiyo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.