Saturday, August 24

AIBU: Upangaji matokeo hadharani ligi ya mkoa Manyara (+video)

0


Mchezo wa ligi ya mkoa wa Manyara kati ya Morning Star dhidi ya Firestone ulioshuhudiwa ukimalizika kwa Morning Star kushinda 8-2, umejaa harufu ya rushwa na upangaji matokeo.

Picha lilivyo

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Babati Gerard Mtui, hatua ya makundi (kulikuwa na makundi mawili) ya ligi ya mkoa wa Manyara ilimalizika salama huku kukiwa hakuna malalamiko yoyote bada ya kila timu kuridhika na kilichotoea kwenye hatua hiyo.

Ligi ikaingia hatua ya sita (6) bora mechi zikapigwa, baadaye kuna timu ikajiondoa kwa hiyo matokeo yote yaliyoihusisha timu hiyo yakafutwa, timu zilizobaki zikasalia na matokeo ambayo hayaihusu ile timu iliyojitoa kwenye ligi.

Majanga yalivyoanza

Kabla ya mchezo unaolalaimikiwa  (Firestone vs Morning Star) Usalama Sports ya Babati ndiyo ilikuwa inaongoza katika hatua hiyo ya sita bora ikiwa na pointi sita na magoli mawili, Firestone na Morning Star pia zilikuwa na nafasi ya kuwa mabingwa mkoa w Manyara. Morning Star ilikuwa ikihitaji ushindi na magoli manne ili kuwa bingwa wakati Firestone walihitaji ushindi na magoli matatu ili wawe mabingwa.

Kwa sababu Usalama Sports (Babati) yenyewe ilikuwa imeshamaliza mechi zake kwa hiyo mechi ya mwisho kufunga ligi kuamua bingwa wa mkoa wa Manyara ilikuwa inazikutanisha Firestone (Kiteto) vs Morning Star (Mbulu).

Mechi yenyewe sasa

“Wakati timu hizo zinacheza (Firestone vs Morning Star) inaonekana tayari zilikuwa zimekaa mezani na kuamua kwa namna gani mchezo uwe na ndicho ambacho baadae kilionekana kwa maana ya kwamba mchezo ulichezwa kwa aina ambayo ukiangalia tangu mashindano yameanza hadi yalipofikia hakukuwa na timu ambayo ilikuwa na mchezo wa aina ile”- Gerard Mtui.

“Magoli ambayo yanafungwa ni mchezaji anaachiwa nafasi, mlinzi wa timu pinzani anampa mshambuliaji mpira ili afunge kisha beki huyo anampongeza mfungaji wa timu pinzani. Inaonesha kulikuwa na mpango kuhakikisha kwamba timu fulani ipate nafasi iende mbele dhidi ya timu ambayo ilikuwa ina nafasi ambayo ndio ilikuwa inaongoza kundi.”

Mwisho wa siku mechi ikamalizika kwa Firestone ikachezea goli 8-2 kutoka kwa Morning Star, huku magoli saba katika mchezo huo yamefungwa ndani ya dakika saba.

Hatua zilizochukuliwa na Usalama Sports

Kumbe timu ya Usalama tayari ilisha ‘nyapianyapia’ kwamba kutakuwa na mizengwe kwenye game hiyo (Firestone vs Morning Star) wakajipanga kwa ajili ya kurekodi mchezo huo ili kuwa na ushahidi.

“Walipata tetesi huenda kungenuwa na mambo ambayo si ya kiungwana kwenye mechi hiyo ili kupata bingwa ambaye hana sifa kwa hiyo Usalama wakaamua kuurekodi mchezo huo, na sio mechi hiyo tu wamesha fanya hivyo kwenye mechi kadhaa,” mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Babati ameiambia shaffihdauda.co.tz.

Baada ya sakata hilo, chama cha soka wilaya ya Bababi kiliishauri Ualama Sports kuandika barua kwenda kamati ya mashindano na chama cha soka mkoa wa Manyara kulalamikia mchezo uliozikutanisha Firestone vs Morning Star kwamba ulikuwa na viashiria vya upangaji wa matokeo.

Tayari Usalama Sports imeandika barua kwenda kamati ya mashindano pamoja na chama cha soka Manyara kwa hiyo wanasubiri uamuzi utakaotolewa.

Utamu upo hapa

Leo Ijumaa Machi 30, 2018 mikoa yote inatakiwa kutangaza mabingwa wake, je manyara wataitangaza Morning Star kuwa ndiyo bingwa?Read More

Share.

About Author

Comments are closed.