Wednesday, August 21

MKURUGENZI WA ELIMU AFRIKA ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WENYE MAHITAJI, JIJINI ARUSHA.

0


KINDNESS CHILDREN CARE, KIJENGEJUU – ARUSHA.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Elimu Afrika Mwl Daniel Urioh ametembelea kituo cha watoto wenye mahitaji, Kata ya Kimandolu, Jijini Arusha.

Ziara hiyo imetokana na ushirikiano wake na Vyombo vyingine vya habari, ambapo Arusha One Radio ya Arusha ilimwalika katika siku ya kutembelea vituo vyenye uhitaji, kimsingi Radio hiyo ualika wananchi kuchangia vitu mbalimbali kama chakula, nguo n.k kila tarehe 25 ya kila mwezi hutembelea kituo kimoja hapa Mkoani Arusha.

Akizungumzia siku hii Mwl Daniel Urioh amesema. ” Ninafuraha kubwa kushiriki siku hii ya Jumapili ya matawi tukielekea pasaka pamoja na watoto hawa wenye vipaji na ujasiri wa kuikabili kesho yao, pia ninaishukuru kwa dhati Arushaone Radio kwa kuamua kufanya jambo hili kubwa lenye thawabu kwa Mungu”.

@ Arusha, TanzaniaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.