Saturday, July 20

Vijana kutoka SOS Village wapata Ukombozi kutoka StarTimes

0Vijana kutoka SOS Village wapata Ukombozi kutoka StarTimesKampuni ya Star Media (T) Ltd na SOS Children’s Villages Tanzania wametia saini makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi, lengo likiwa ni kuwapatia fursa  mbalimbali hasa kiteknologia ili kuendana na malengo ya Milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Katika mkataba huo StarTimes itakuwa ikisaidia programu mbalimbali za SOS Children’s Village katika mikoa zaidi ya saba (Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Iringa na Mufindi) hasa kwenye kupanua nafasi za kujifunza na kukuza uzoefu miongoni mwa Vijana wa SOS Children’s Village.

Moja ya mambo ambao StarTimes itafanya ni kuwapatia nafasi Vijana kutoka SOS Villages Tanzania bara na Zanzibar kujifunza kwa vitendo kazi mbalimbali zilizopo kwenye kampuni yao, ushauri, mafunzo ya kiufundi kuhusu namna ambavyo StarTimes inafanya kazi hasa katika Idara ya Masoko na kuhusu bidhaa zake ili kukuza uelewa wa kazi na ajira kwa Vijana.

 

 

 

Ushirikiano wa StarTimes na SOS Children’s Village utasaidia kwa kiasi kikubwa kutengeneza Vijana ambao wataweza kuingia katika soko la ajira ili kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ukosefu wa ajira.

Mbali na hayo wafanyakazi wa StarTimes pia watapata nafasi ya kushiriki na Vijana wa SOS Children’s Village katika shughuli mbalimbali ikiwemo michezo na wakati kushiriki katika kuchangisha fedha ili kusaidia Vijana hao katika kuendeleza ndoto zao na kufanikiwa zaidi.

Comments

comments
Share.

About Author

Leave A Reply