Monday, August 19

UEFA yatangaza Mabadiliko 2018/2019, Yaongeza idadi ya ‘Sub’ Muda wa nyongeza.

0


Kuelekea Msimu Ujao 2018/2019 wa Michuano ya UEFA Champions League na EUROPA League, Uefa imetangaza mabadiliko mengine ukiachilia mbali kuruhusu timu nne za Ligi kubwa kufuzau Moja kwa Moja.

Siku ya Leo Uefa imetangaza Mabadiliko mengine ambayo yatazipa Timu zote zinazoshiriki Michuano hiyo Upana wa kufanya Mabadiliko, Msimu huu na Misimu iliyopita katika hatua ya mtoano ya Michuano hiyo Timu ilikua na Jumla ya Wachezaji 18 (11 Uwanjani na 7 kwenye Benchi) huku Wachezaji watatu tu kutoka Benchi ndio walikuwa wanapata nafasi ya kuingia Uwanjani kwenye Mabadiliko(Substitution) lakini kuanzia Msimu Ujao sheria mpya imetangazwa, kwanzia Msimu huo kwenye hatua ya Mtoano pekee Timu inayocheza itakuwa na Jumla ya Wachezaji 23 (11 Uwanjani na 12 Benchi) ikiwa ni Ongezeko la Wachezaji Watano kwenye Benchi.

Mabadiliko mengine ni Ongezeko la Sub katika Dakika za nyongeza, Awali timu zilikua zinaruhusiwa kufanya Sub tatu tu mpaka Mpira unamalizika lakini kuanzia Msimu ujao Timu zitaruhusiwa kufanya Sub nne yaani Mchezaji mmoja zaidi katika Muda wa Nyongeza (Dakika 120).

Mabadiliko hayo yatatumika katika hatua ya Makundi na Mtoano pekee ila kwenye hatua ya Fainali ya UEFA Champions na EUROPA pamoja na Mchezo wa Ubingwa wa Super Cup hayatatumika.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.