Wednesday, August 21

Manchester United yakubaliana na Zlatan Ibrahimovic kuvunja Mkataba

0


Kweli kila Lenye Mwanzo halikosi kuwa na Mwisho! Hayo ni baadhi tu ya Maneno kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya Siku ya Jana Klabu ya Manchester United kutangaza kufikia Makubaliano na Mchezaji huyo ya kuvunja Mkataba kwa Maslahi ya Pande zote mbili.

Zlatan Mwenye umri wa Miaka 36 alijiunga na Mashetani hao wekundu akitokea nchini Ufarasa katika Klabu tajiri ya PSG Julai Mosi Mwaka 2016 akiwa kama mchezaji huru

Alijiunga na United ambayo ilikuwa haijashinda Kombe la Ulaya kwa Takribani Miaka 11, Msimu wake wa kwanza ndani ya United alifanikiwa kuisaidia Timu yake kushinda Taji la Europa kwa mara ya kwanza katika Historia ya Klabu hiyo, lakini pia aliisaidia United kunyakua ubingwa wa Kombe la EFL cap  Februai 26 dhidi ya Southampton akifunga Magoli mawili kwenye ushindi wa MAGOLI MA 3-2.

Akiwa na Uzi wa United Zlatan amecheza Jumla ya Michezo 53, akifunga magoli 29 pamoja na kutoa assist 10. Inaripotiwa kuwa Zlatan anaelekea nchini Marekani kucheza katika klabu ya LA Galaxy inayoshiriki Ligi kuu nchini Humo, Bila shaka nyakati zake za kutamba zimefikia ukingoni sasa, ameshinda Mataji mengi sana katika Klabu Tofauti alizowai kutumikia ameifanya United angalau kuwa ile United ya zamani, Bila shaka kila Shabiki wa Man U ameridhika na kile alichokifanya Mchezaji huyo ndani ya  Klabu hiyo.

 

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.