Tuesday, July 23

Arsenal kuendeleza Ubabe wao EUROPA?

0Arsenal kuendeleza Ubabe wao EUROPA?


during the UEFA Europa League Round of 16 Second Leg match between Arsenal and AC Milan at Emirates Stadium on March 15, 2018 in London, England.


Katika mechi ya nne ya hatua ya makundi kwenye ligi ya EUROPA Alhamisi hii timu ya Arsenal itakuwa nyumbani katika dimba la Emirates dhidi ya Sporting CP ya Ureno. Katika mchezo wao wa mzunguko wa kwanza Arsenal waliibuka na ushindi wa bao 1 ambao uliwawezesha kuwa vinara na kuongoza kundi E.

Arsenal wamekuwa katika kiwango bora na wanacheza kandanda safi tangu wampate kocha Unai Emery ambaye amebadilisha aina ya uchezeji wake. Mchezo huo utachezwa Alhamisi tar 8 Novemba, majira ya saa 5:00 Usiku saa za Afrika Mashariki.

Usiku huu wa EUROPA mechi nyingine zitakazochezwa ni pamoja na ule wa Chelsea ambao watakuwa ugenini dhidi ya BATE Borisov (saa 2:55 Usiku), Fenerbahce vs Anderlecht (saa 12:50 jioni), Lazio vs Olympique Marseille (saa 2:55 Usiku), Celtic vs RB Leipzig (saa 5:00 Usiku) na Real Betis vs AC Milan (saa 5:00 Usiku).

kumbuka Michuano ya EUROPA inaonyeshwa moja kwa moja kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee kupitia chaneli mbalimbali ikiwemo ya ST World Football. StarTimes pia wanaonyesha ligi ya Bundesliga pamoja ile ya Ufaransa, maarufu kama Ligue 1. Katika Bundesliga wikiendi hii kuna mchezo mkubwa ambao unafahamika kama Der Klassiker unaokutanisha miamba miwili, wazee njano na nyeusi Borussia Dortmund watawakaribisha Bayern Munich katika dimba la Signal Iduna Park saa 2:30 Usiku jumamosi hii, kumbuka Dortmund ndio vinara wa ligi hiyo baada ya kuanza vizuri msimu huu wakiwa hawajapoteza mchezo wowote hadi sasa. Bayern ambao wamesuasua sana msimu huu hivyo watakuwa na kibarua kigumu kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Dortmund.

Comments

comments
Share.

About Author

Leave A Reply