Tuesday, August 20

Aish Manula, John Bocco kuikosa Gendarmarie

0


Golikipa nambari Moja wa Simba Aish Salumu Manula pamoja na Nahodha John Raphael Bocco watakosekana katika Mchezo wa Leo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Klabu ya Gendermarie ya nchini Djibout kufuatia kusumbuliwa na Majeruhi.

Bocco ambaye alifunga Magoli Mawili katika Mchezo wa kwanza aliumia sehemu ya Kifundo cha Mguu wa Kushoto katika Mchezo wa Ligi dhidi ya Mwadui ambao Simba ilitoka sare ya 2-2 huku Manula akijitonesha sehemu ya kidole cha Mkono ambacho aliumia pia kwenye Mchezo huo dhidi ya Mwadui.

kuwakosa Bocco na Manula ni pigo kubwa kwa Wekundu wa Msimbazi ukiangalia Mchango wa Wachezaji hao katika kikosi, Bocco amefunga Magoli 10 katika Ligi huku akifunga Magoli mawili mpaka sasa katika kombe la Shirikisho. Manula amekuwa katika kiwango kizuri kwenye Ligi akiwa ni Golikipa aliyeruhusu wavu wake kuguswa mara chache huku akiisaidia Simba katika Mchezo uliopita kwa kuokoa Penati dhidi ya Djibout.

Simba ilisafiri na Golikipa wa akiba ambaye ni Emmanuel Mseja ambaye atachukua nafasi ya Manula huku nafasi ya Bocco itategemea na uchaguzi wa kocha kulingana na kikosi chake. Simba inashuka Uwanjani Leo Februari 20 2018 katika Dimba la State de Vile wenye uwezo wa kuingiza Mashabiki 40,000.

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.