Sunday, August 25

Zimwi la Ualimu laangukia ‘Post’ ya Timbulo

0


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania na Straa wa ngoma ya ‘Mfuasi’, Timbulo amezungumzia kuzingatia kinachomkumbusha taaluma yake ya ualimu na maudhui ya kinachoonekana katika video ya wimbo wake mpya kwa jina ‘Post’.

Akijibu swali la muandiko kwa chaki ubaoni kwa namna inavyoonekana katika video ya wimbo wake huo, Timbulo amesema kuwa Taaluma ya ualimu kwake inabaki kuwa ni kazi aliyoipeda sana na katika video ameona sio mbaya kama atawasilisha hisia zake kwa sehemu ya muonekanao wa taaluma hiyo.

“Dah hili ni swali la maisha yangu na naamini mashabiki wanakumbuka kuwa Timbulo mbali na kupenda muziki wanajua kuwa anapenda taalkuma yake ya wali. Katika hii video kwa kinachoonekana ni katika kuwasilisha mapenzi yangu kuelekea taaluma yangu nah ii nikiwa kama msanii mwenye kutumia sanaa yangu nimewasilisha hisia zangu kama ninavyoweza kuwasilisha hisia za mashabiki zangu au mtu mwingine”  Amasema Timbulo.

Timbulo kazi yake ya mwisho aliiachia mwishoni mwa mwaka kwa jina ‘Vibaya’ na wimbo huu mpya umendaliwa na Prodyuza Mocco Genius na Video imeongozwa na Director Lucca Swahili.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.