Thursday, August 22

Willy Paul atoa sababu za kumtumia Lynn wa Kwetu kwenye video yake mpya

0


Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Wilson Abubakar Radido ‘Willy Paul’ ameachia kazi yake mpya chini ya lebo yake ya ‘Saldido Records’, iliyotayarishwa na Prodyuza Teddy B na ametoa sababu za kwanini amemtumia Mrembo na Video Vixen ‘Lynn’ kutoka Tanzania katika video ya wimbo huo.

Akipiga stori na Dizzim Online, Willy Paul amesema kuwa, siku zote kitu kikubwa anchozingatia katika kazi zake ni kufanya kazi nzuri na kubwa yenye viwango vya kupimwa kimataifa na moja ya sababu ya kumshirikisha Lynn kama video Queen kwenye video ya wimbo wake huo mpya ni ‘Urembo’ aliobairikiwa nao binti huyo.

“Asante sana kwa Support ninayopata kutoka kwa mashabiki na wadau wa music kwa huko Tz coz wana mchango wa mimi kufika hapa, on my new Project. I am very proud of Lynn wa kwetu kushiriki katika video yangu and what I can say about her ni mrembo na pia hiyo ni one of my reasons mimi kufanya naye kazi” Amesema Willy Paul.

Video ya wimbo huo iliongozwa na Director Hanscana kutoka Tanzania na imeshootiwa mjini Mombasa, Kenya.

Itazame Video hiyo mpya hapaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.