Wednesday, August 21

Willy Paul anaweza kuachia wimbo mpya kuazia sasa, Je, itakuwa ni kolabo?

0


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya na Mmiliki wa Stduio na lebo ya muziki ya Saldido Records, Wilson Shikwekwe Radido a.k.a Willy Paul ameonekana katika dalili za kuachia wimbo Mpya na idadi kubwa ya mashabiki wameanza kuhisi kuwa ujio ni kolabo ya Staa huyo na Staa kutoka Tanzania.

Willy Paul akiwa katika Studio zetu

Itakumbukwa mwezi huu katika mahojiano yetu na Willy Paul, alisema kuwa baada ya ngoma yake ya ‘Malingo(Maringo)’ itegemewe kolabo kutoka kwake na hii ilikuja baada ya kusema kuwa tayari wimbo wake na Staa wa Bongo Fleva, Harmonize imekamilika na kilichobaki ni kushoot Video ya wimbo wao na sasa taarifa za chini chini ni kuwa kuna uwezekano washashoot video ya kolabo.

Willy Paul na Harmonize wakiwa Set

Kilichoonekana ni Muda mfupi baadae kuelekea uzinduzi wa Album ya  ‘A Boy From Tandale’ uliofanyika nchini Kenya, Wasanii wote wa lebo ya WCB Wasafi isipo kuwa Rayvanny aliyekuwa ziarani nje ya nchi, walisafiri kuelekea kwenye uzinduzi huo kumsindikika Diamond Platnumz na Harmonize akiwa nchini Kenya, Willy Paul alipost picha zake na kati ya picha hizo ipo aliyopost akiwa na Harmonize katika maudhui ya kuwa walishoot Video.

Willy Paul akiwa na Vanessa Mdee katika Pozi walipokutana nchini Tanzania

Mapema leo Willy Paul amepost picha yeke akiwaomba mashabiki ruhusa ya kuachia wimbo mwingine au asubirie.

“Should I drop it now ama i wait kidogo?” Willy Paul Aliandika.

Na moja kwa moja imehisiwa kuwa kuna uwezekano ikawa ni kalabo yake na Harmonize au Staa mwingine kwakuwa kwa kipindi alichokuwa Tanzania mbali na kukutana na Mastaa kama Vile Ben Pol na wakafanya kazi pia alikutana na Vanessa Mdee na Mastaa wengine.

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.