Thursday, August 22

Sean Kingston awavuta Davido na Tory Lanez kwenye ngoma moja

0


Rapa, Mwimbaji, mwandishi, na mtunzi wa kazi za muziki kutoka Marekani, Kisean Anderson ‘Sean Kingston’ amefichua juu ya ujio wa kazi yake mpya itakayomshirikisha Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido na Staa wa muziki Mkanada, Tory Lanez.

Davido na Tory Lanez

Jumamosi ya tarehe 17, kupitia mtandao wa Twitter, Kingston aliweka ujumbe kuwa kazi iliyoko njiani kutoka kwake inakwenda kwa jina la ‘Kryptonite’ na Afrika imewakilishwa na Davido katika wimbo huo, huku isibainike kama Tory Lanez karap, kaimba au kafanya mchanganyiko kwakuwa anaweza kote kote.

“My new single Kryptonite ft @torylanez x @iam_davido it’s on the way Currently getting Mixed & Mastered  !!!!” alitweet Sean Kingston.

Hata hivyo kwa Davido kolabo hii haitakuwa mara yake ya kwanza kufanya na Staa au Mastaa wa Kimataifa kwakuwa alishafanya kazi na Tinashe, Meek Mill na Rae Sremmurd na Young Thug kwenye ‘Pere’ iliyotolewa hivi karibuni.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.