Sunday, August 25

Rayvanny atupia taarifa za kolabo yake na Nasty C

0


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Staa wa ngoma ya ‘Makulusa’ kutoka Tanzania, Raymond Shaban Mwakyusa a.k.a Rayvanny amethibitisha kuwa ana kolabo na rapa kutoka Afrika Kusini, Nasty C kupitia video waliyoonekana wakiwa Studio za Wasafi Records.

Rayvanny anayefanya muziki wake chini ya lebo ya studio hizo amethibitisha kolabo yake na Nasty C kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa video iliyowaonesha wakirekodi Studio katika hali ya kurekodi.

@Rayvanny X @nasty_csa #SUBSCRIBE #YOUTUBE #RAYVANNY

A post shared by Raymond (@rayvanny) on Mar 21, 2018 at 3:14am PDT

Kwa mara ya kwanza Nasty C alipotua Tanzania alisema kuwa alikutana na Rayvanny mjini Los Angeles, Marekani.

Msanii mwingine kutoka Tanzania ambaye alishakutana na rapa huyo ni Staa wa ngoma ya ‘Kivuruge’, Nandy ambaye kwa mujibu wa Nasty C mwenyewe aliosema kuwa angependa kufanya naye kazi.



Read More

Share.

About Author

Comments are closed.