Sunday, August 18

Nisha Afunga Mkataba wa Mapenzi na Brown, Aamua kuwa Bachela

0


Muigizaji kutoka Bongo Movie, Salma Jabu maarufu kwa jina la ‘Nisha Bebe’ baada ya kuhisiwa kuwa anatoka kimapenzi na Brown ambapo katika Post zake zote hasa kupitia ukurasa wake wa Instagram hakusahau kuambatanisha hashTag ya Neno #Bachela sasa ameachia video ya wimbo ambayo yeye niye anayesikika akiimba na Brown ametokea katika video kama Video King.

Brown ambaye katika kifua chake amechora tattoo ya ‘I love Wolper’ alionekana kuwa ameifunika kwa kuchora  tattoo nyingine na Nisha amethibitisha kuwa Deal Done na kubainisha ilikuwa ni ujio wa wimbo wake wa #Bachela.

Aliandika kwenye ukusa wake wa Instagram kuwa ‘@nishabebee: “deal done its all about #BACHELA link on my bio 👆 (mabibi na mabwana karibuni kutazama kazi yangu mpya #BACHELA BONYEZA LINK HAPO JUU kwa full video NA USISAHAU KUSUBSCRIBE na KUSHARE😙)”.

Kwa Nisha kuandika hivyo inahisiwa kuwa tattoo hiyo ya Brown ya kufunika Tattoo yake ya awali ya ‘I love Wolper’ ni Tattoo ya muda kwakuwa Nisha amesema kuwa ‘Deal Done’ yaani Isingeleta maana kama Brown angetokea katika Video ikiwa eneop la kifua chake tattoo ikionekana na ni yenye kuzungumzia jina la mtu mwingine ambaye hahusiki kwa vyovyote katika wimbo huo wa Nisha.

Wimbo huo mpya wa Nisha umetayarisha katika Studio za Moja Moja Records kwa mkono wa Prodyuza Zest.

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.