Friday, August 23

Marioo anasimulia Maisha yake na Mpenzi wake ndani ya Masaa yasiyozidi 12 na Alishindwa kuonana naye ndani ya miaka 5

0


Msanii wa muziki wa kizazi kipya na muandishi wa nyimbo kutoka Tanzani, Marioo alianza kutiliwa maanani baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Dar Kugumu’ ingawa Alisha anza kuzungumzwa na wachache kwa ushiriki wake wa kuandika wimbo uliofungiwa wa msanii Gift a.k.a Gigy Money ‘Nampa Papa’.

Dar Kugumu ni wimbo uliopata mapokeo mazuri sana na zaidi kilichopendwa na idadi kubwa ya walioupokea ni wazo la wimbo linaloeleza penzi la muda mrefu katika ya Marioo na Mrembo aliyeachwa kijijini kwa safari ya utafutaji ya kwenda mjini kwa muda usio pungua miaka mitano.

Kwa muda wote huo, Marioo alifanikiwa kwa kupata chombo cha usafiri cha miguu miwili ambacho katika simulizi ya video inaonekana katika usiku mmoja wa maisha yake ya utafutaji alikumbana na tukio la kuibiwa usafiri wake huo na katika uandishi alibainisha hali hiyo kama changamoto tu ambapo mpaka anakutana na mpenzi wake alikuwa namiliki usafiri wa miguu mitatu maarufu kama Bajaj.

Kinachosikika katika wimbo huu na mfuatano wa matukio katika video ni kukimbia kwa masaa na simulizi nzima inaonekana kusimulia tukio la kumbukumbu chache za maisha ya nyuma na siku moja ambayo ni ya Marioo kumtafuta mpenzi wake kwa simu na kukuta namba imefungiwa, hatua iliyofuata ni Marioo kumuandikia barua Mpenzi wake siku hiyo na siku hiyo hiyo ilimfikia akiwa katika shughuli za hapa na pale za kila siku pale kijijini na baada ya kuipata alifuata hatua ya kuazima simu na kumpigia Marioo.

Marioo anasikika katika wimbo akimuelezea mpenzi wake hali ilivyona unafuu kwa kipindi hiki tofauti na kipindi cha nyuma na siku hiyo hiyo Marioo alikuwa kazini anafanya hayo yote na kwa mujibu wa simulizi ya video ya wimbo huyo ni kuwa siku hiyo hakufanya kazi yoyote bali alikuwa akimsubiria Mpenzi wake kutoka kijijini ambaye anamuagiza aage majirani na kumbebea Miogo kwakuwa ni siku nyingi tangu ametumia aina hiyo ya Chakula. Siku hiyo hiyo Mrembo anapanda Gari na kuanza safari kuelekea mjini kukutana Mpenzi wake huku Marioo akimgojea Stendi ya Mabasi na siku hiyo hiyo safari ikikamilika na wakakutana kwa furaha kubwa mapema mchana.

Bila shaka safari ya Mrembo wa Marioo ilikuwa fupi sana kiasi amabacho siamini kama angeamua kutumia usafari wake hata kwa kuunga unga angeshindwa kifika kuwasalimia wanafamilia pamoja na mpenzi wake kwakuwa safari ya kutoka kijijini kwenda mjini iliwezekana na iliwekzekana ndani kuishuhudia safari mbili za kimahusiano katika mawasiliano ya wapenzi hao.

Simulizi hii inatonesha kuwa kutokana na teknolojia mambo yanawezekana kwa uharaka zaidi lakini kwa uhalisia hili limewezekana kwa kasi kubwa sana kwa kuwa yote yamewezeakan kutusimulia maisha ya wapenzi kukutana kutoka kijijini mpaka mjini ndani ya siku moja mbali na kuwa wanapitia changamoto ndogo ndogo za kimawasiliano.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.