Friday, August 23

Eddy Kenzo Awachakaza Diamond Platnumz, Davido, Cassper Nyovest na Mastaa wengine

0


Staa wa muziki kutoka nchini Uganda, Edrisa Musuuza ‘Eddy Kenzo’ amewagalagaza Diamond Platnumz kutoka Tanzania, Cassper Nyovest wa Afrika Kusini, mwanamichezo Caster Semenya wa Afrika Kusini, mwimbaji Davido kutoka Nigeria na mtoto mwigizaji maarufu ‘Emmanuella’ kutoka Nigeria katika usiku wa tuzo za Nickelodeon Kids’ Choice Awards 2018.

Mshindi huyo wa Tuzo ya BET International Viewers’ Award ya mwaka 2015, alitangazwa kama mshindi wa tuzo hiyo ya Nickelodeon Kids’ Choice Awards kwa mwaka huu katika kipengele cha Favorite African Star katika utoaji wa Tuzo hizo zilizofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi The Forum mjini Inglewood, jimbo la California na Ushindi kwa Eddy Kenzo ambao kwa wiki kadhaa umekuwa ni muendelezo wa ushindi kwake.

Wikiendi mbili zilizopita Upande mwingine Eddy Kenzo alishinda Tuzo ya ‘Best African Entertainer’ katika toleo la 36 la International Reggae and World Music Awards (IRAWMA) zilizofanyika Logan Center katika mji wa Chicago, Marekani.

Baada ya Ushindi wa Kinds Choice Awards.

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.