Monday, August 19

Dalili za Birdman na Lil Wayne zinazidi kufichuka

0


Rapa, Mtayarishaji na Mfanyabiashara kutoka nchini Marekani, Bryan Williams a.k.a Birdman amezidi kuonesha kuwa hana tofauti tena na Msanii mwezake na rafiki wake wa Siku Nyingi, rapa Dwayne Michael Carter, Jr. ‘Lil Wayne’.

Staa huyo mmiliki na mualianzishi wa studio na lebo ya muziki maarufu kama Cash Money Records aliweka picha kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na  Lil Wayne na kuandika ujumbe wa kuonesha wawili hao kwa sasa hawana tatizo kabisa na wako tayari kuwa wanaweza kufanya chochote cha kibiashara.

“Me and My Son #YMCMBEAST” na Maoni ya wengi walioneakan kupendezwa sana akiwemo Drake ambaye aliweka maoni ya kuonesha kufurahishwa na urafiki wa wawli hao na kuweka ishara ya kubariki ukaribu wao.

Dalili za kumalizika kwa tofauti za wawili hao ni pale walipokutana katika kiwanja kikubwa cha Starehe mjini Miami mapema mwezi huu ambapo alionekana kwakikumbatisha na kuzungumza kwa kusikilizana kwa umakini na hali inakuja sambamba na wadau wa kungoja ujio wa Album ya The Carter V iliyoko mikononi mwa Birdaman na inaweza kuachiwa muda wowote kuazia sasa.

Me and my SON #YMCMBEAST

A post shared by Birdman5star (@birdman5star) on Mar 26, 2018 at 2:16am PDTRead More

Share.

About Author

Comments are closed.