Wednesday, August 21

Cassper Nyovest na Stone Boy wachanganya ujuzi wa muziki wao nchini Ghana

0


Rapa, Staa wa muziki na Mzaliwa wa nchini Afrika Kusini, Refiloe Maele Phoolo a.k.a Cassper Nyovest kwa sasa yuko nchini Ghana na kinachoonekana kwa sasa ni kuwa amefanya kolabo ya wimbo na Mkali wa ngoma ya ‘One Thing’, Livingstone Etse Satekla a.k.a Stone Boy.

Tangu kufika kwake nchini humo siku ya Jumapili Machi 25, Cassper amefanya ziara ya kimuziki kwenye vyombo vya habari kadhaa na ziaidi amesika akifafanua uzoefu wake nchini humo na kukua kwa muziki wa Afrika kwa ujumla kiasi cha wasanii baadhi Afrika kuweza kutambulika katika mataifa ya Mbali.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Cassper aliweka picha akiwa na Stone Boy wakiwa Studio na kuandika

@casspernyovest:”Made a smash last night!!!! BHIM NATION WORLDWIDE!!!!! @stonebwoyb

Stone Boy naye alishindikia Msumari juu ya ujumbe wa kolabo yake na Cassper Nyovest kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuweka picha yake akiwa na Rapa huyo na kuandika.

@stonebwoyb: Made A Smash Last Night 💥#NyovestNation @casspernyovestRead More

Share.

About Author

Comments are closed.