Sunday, August 25

Bugalee alilia kupostiwa na Mastaa wakubwa Afrika

0


Mtayarishaji na msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Bugalee amesema kuwa kinachokwamisha wasanii baadhi katika muziki nchini Tanzania ni kutopata mchango wa kutangaza kazi zao katika mitandao ya kijamii ili waweze kufahamika zaidi kupita sanaa yake.

Akizungumza na Dizzim Online, Buga amesema kuwa kwa sasa asilimia kubwa nje ya nyimbo uchezwa katika vyombo vya habari kama njia ya kuutangaza na kutangaza majina ya wahusika, zaidi uwasanii wamekuwa wakitegemea sana mitandao ya kijamii na anaamini kupostiwa mara kwa mara na wasanii wenza na wadau wakubwa juu ya kazi husika ni moja ya support kubwa inayoweza kuutangaza muziki wa msanii na kazi za utayarishaji kama ilivyo kwake.

“Mimi naamini kila mtu kwa sasa hasa wasanii kama mimi, tunategemea sana mitandao ya kijami na hilo halipingiki. Sasa mimi nimefanya wimbo wang mpya kutokana na hali halisi ya kimuziki na kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii, wimbo wangu mpya umezingatia hili ingawa watu wanaweza kuichukulia Serious lakini ile ni sanaa tu na kwa kaisi kikubwa mtu akisikiliza atapata burudani na hilo ndo lengo” amesema Bugalee.

Hata hivyo Buga amekuwa akionekana zaidi katika muziki kama msanii mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu na jibu la msanii kutegemea zaidi mitandao ya kijamii alilijibu alipokuwa akizungumzia wimbo wake mpya kwa jina ‘Ni Post’.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.