Wednesday, August 21

Beka Flavour na Mr Blue waanika nguo bila vibanio

0


Ni wakali wawili kutoka Tanzania, wamekutana katika kolabo ya pamoja na Beka Flavour anajitokeza katika  kumsifia na kuweza wazi mapenzi yake kwa mrembo kiasi cha kutaka wafanane ambapo katika hilo anaungana mkali wa uandishi na michano ya kutoa sifa za upendo na urembo kwa akina dada Mr Blue katika ngoma mpya kwa jina ‘Tuwesare’.

Beka na Byser wanawakilisha kwa uzuri na sifa za kumpenda mpenzi kwa uandishi na Michano iliyopatikana katika ngoma hiyo iliyotayarishwa kwa ufundi wa kisanaa na Prodyuza Maximizer.

Video ya wimbo huo imeongozwa na Director wa kifaransa kwa jina ‘Kader Alassane’ chini ya kampuni ya Over Dreamz Pictures na katika simulizi na kuuvaa uhusika wa wimbo huo imeonekana kuwa Beka Flavour  ni kijana muangaikaji wa maisha ya kutafuta kipato kutokana na kazi zake za kujiajiri na ana maisha ya kati ambapo Byser Alibaki katika muonekano wa Uvaaji wa kitanashati tu.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.