Tuesday, August 20

Beka Flavour amsindikiza Bonge la Nyau, waongozana kwenda safari ya mbali

0


Staa wa muziki kutoka Tanzania na mkali wa ngoma ya ‘Aza’, Bonge la Nyau ‘Nyauloso’ ameachia kazi yake mpya ikiwa ni yenye kumshirikisha Muimbaji Beka Flavour chini ya utayarishaji wa Studio za Kiri Records kwa mkono wa Prodyuza Bear.

Ngoma hiyo inayokwenda kwa jina ‘Najiona Mbali’, Beka amepiga Chorus kwa ufundi na kumuachia nafasi Nyauloso msifie mrembo kwa michano yenye mchanganyiko wa melody za kuimba ambapo video ya wimbo huo kuongozwa na Director Joowzey kutoka Joh Film.

Bongela Nyau amekuwa na utaratibu wa kuhakikisha anawashirikisha wakali wa kuimba kwenye kazi zake kwakuwa katika kipindi chote cha yeye kufanya vizuri ameshawashirikisha mastaa wakubwa ambao ni pamoja na AliKiba, Barnaba, Q Chief ‘Q Chillah’, Barakah The Prince, Bob Junior  na Beka Flavour.

Itazaame video ya wimbo huo mpya.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.