Tuesday, August 20

AY na mpenzi wake Remmy wafunga ndoa jijini Dar es Salaam

0


Staa wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Ambwenne Yessaya ‘AY’ amefunga ndoa na mchumba wake Rehema Sudi Suleiman ‘Remmy’ rasmi siku ya leo jijini Dar es Salaam katika hoteli ya kifahari ya Golden Tulip na tukio hilo limeudhuriwa na marafiki wake wa karibu, na wadau wa muziki kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Chumba cha habari cha Dizzim Online kilizidaka taarifa za wapenzi hao kuwa watafunga ndoa nchini Tanznaia mapema wiki hii na mapema leo kufanikiwa kunasa video na picha za tukio hilo la ufungaji  ndoa ambapo miongoni wa walioonekana kuwa sehemu ya tukio hilo ni pamoja na rapa Fid Q, B Dozen, Professor Jay, Mwana FA, Salama Jabir, Prodyuza wa muziki Hermy B, wadau wa muziki kutoka nchini Kenya, Mtangazaji Shaffie Weru na Mwanamitindo Fundi Frank.

Hakika mwaka wa 2018 umekuwa ni wa AY na Remmy kugongelea nyundo juu ya penzi lao na kukamilisha hatua zote za kuwa mke na mume kwakuwa tarehe 10 ya mwezi Februari mwaka huu AY alikamilisha zoezi la utoaji mahari mbele ya wazazi na hatimaye pingu za maisha ya wawili hao zimefungwa na kuandika historia ya kuwa wataishi pamoja katika shida na raha.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.