Thursday, August 22

Arrow Bwoy azidisha shukrani tele kwa King Kaka

0


Msanii wa muziki  Danso kutoka nchini Kenya, Arrow Bwoy amezidi kumshukuru zaidi Mshairi, rapa na Staa wa muziki nchini humo, Kennedy Ombima a.k.a Kaka Sungura ‘King Kaka’, kwa msaada mkubwa wa kimuziki alioupata na anaozidi kuupata mpaka sasa katika ujio wa ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Shikisha’.

Arrow Bwoy

Akizungumzia jitihada na changamoto zake katika muziki, Arrow Bwoy amesema kuwa kwake ilikuwa ni bahati kubwa sana kujikuta katika mikono ya Kaka Sungura anayemiliki lebo ya muziki ya Kaka Empire inayosimamiza muziki wake na wasanii kama vile Femi One, Avril, Timmy T Dat na wasanii wengine chini ya lebo hiyo..

“Ndoto nilikuwa nayo ilikuwa ni kubwa ya Muziki… so nikaona acha nizidi, kuzidi nikaingia Group inaitwa FastCash Music Group so we have been doing our things all over suddenly Kaka came in…Nilikutana na Kaka hapa Westie(Westland) ilikuwa Skyluxx Bash ya Owago Onyiro so that Day I was given a Platform to Perform, kuna ngoma niliperform Kaka akapenda sana akanifatilia akaomba number yangu kidogo nikasikia amenitext manzee nilifurahia sana unajua to get messege from one of the humbling and hardworking guy in the industry anakwambia yaani tufanye kazi  that was a win for me” Amesema Arrow Bwoy alipokuwa akiongea na The Cruz ya EA Radio.

Rabbit Kaka Sungura ‘King Kaka’

Arrow Bwoy anayefanya vizuri kwa sasa na ngoma yake ya ‘Shikisha’ alishapamba moto katika vyombo vya habari kwa ngoma kama vile ‘Digi Digi(Go Down)’, ‘Koona’, ‘Bila Bonus’ na ‘Murder’ zilizofanya vizuri sana na kuwafanya waliowengi kuanza kuamini katika kipaji na muziki wa msanii huyo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.