Sunday, August 25

Akothee Ajiongezea Staa mwingine mkubwa Afrika

0


Msanii wa muziki kutoka Nchini Kenya, Esther Akoth a.k.a Akothee ameachia kolabo ya wimbo wake mpya kwa jina “OYOYO” akiwa amemshirikisha Mwimbaji kutoka Nigeria, Innocent Udeme Udofot a.k.a McGalaxy, wimbo uliotayarishwa na Prodyuza kutoka Nigeria, Ben’Jamin Obadje a.k.a Spellz.

Video ya wimbo huo mpya ya Akothe Na Mc Galaxy imeshootiwa nchini Kenya na imeongozwa chini kampuni ya video ya nchini Kenya ya ‘One Montage Filmworks’.

Akothee kwa kolabo hii ameongeza idadi ya Mastaa wakubwa Afrika aliowashirikisha katika muziki wake kwakuwa alishashirikiana na Mr. Flavour kutoka Nigeria, OC Osilliation kutoka Zambia na Diamond Platnumz kutoka Tanzania.

Itazame Video ya Wimbo mpya wa Akothee Ft, Mc Galaxy.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.