Monday, August 19

2 Baba apingana na Rais Muhammadu Buhari juu ya mauaji ya wachungaji wa Fulani

0


Mwimbaji kutoka Nigeria, Innocent Idibia a.k.a 2 Baba, ameonesha kutofurahishwa na hatua za utawala wa Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari kutokana na serikali yake kutochukua hatua dhidi ya waasi wa Boko Haram na wachungaji wa Fulani.

Akizungumza na GoldmyneTV mjini Lagos mchini Nigeria, 2 Baba amesema, “Serikali ya Shirikisho haijishughulishi kwa chochote, hakuna kitu kilichofanyika na tunapozungumza, wachungaji wanaweza kushambulia wakati wowote. Serikali ya Shirikisho wanaishia tu kulaumu juu ya mauaji bila kusfanya chochote.

“Inanisikitisha sana ninaposoma juu ya mauaji yasiyo na maana yanayotukia kila siku huko Benue, sio juu ya hali yangu peke yake, hutokea katika nchi nyingine pia na mimi huwasihiana na watu wa Nigeria. Watu hawa ni wahalifu na mashirika ya utekelezaji wa sheria hawaonekani kufanya chochote dhidi ya hilo.

“kwa mimi sijaona juhudi kubwa za kushughulikia suala hili. Wanaijeria wamechoka na ni wenye hasira lakini sisi ni watu wenye upendo na amani, nchi haijaendelea. Wanajua hatuwezi kufanya chochote. ” 2 Baba aliongeza.

Kwa mujibu wake 2 Baba alishauri kuwa itakuwa ni busara endapo Gavana wa Jimbo la Benue, Bw. Samuel Ortom, kuwaambia watu wake wajikinge wenyewe.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.