Friday, July 19

EXCLUSIVE: OTILE BROWN NDIYE MWANDISHI WA NGOMA NALIA YAKE VERA SIDIKA!

0EXCLUSIVE: OTILE BROWN NDIYE MWANDISHI WA NGOMA NALIA YAKE VERA SIDIKA!Otile Brown na Vera Sidika wanatambulika kwa drama yao ya mapenzi, inayowavutia watu lukuki katika tasnia ya burudani Africa Mashariki. Lakini pia inashukiwa kuwa wapenzi hawa wamegundua siri ya maisha ya ustaa, nakutumia fursa hiyo ili kujitangaza zaidi kwa kuwavutia mashabiki ama wafuasi kutokana na mbinu ya kueneza propaganda ama kwa lugha ya maarufu kiki. Otile Brown na Vera Sidika wanafahamu fika kuwa kunao baadhi ya mashabiki ama wafuasi wao ambao hawapendi kuwaona pamoja, huku pia kunao wanao penda sana kuwaona wapenzi hawa wawili na mastaa wakiwa pamoja. Duru za kuaminika kutoka kwa mtu wao wa karibu zinasema kuwa mastaa hawa wawili kutoka nchini Kenya, wanafaidika na kiki hizi kujitnagaza zaidi kibishara. Na licha ya kusambaa kupitia mtandaoni kuwa wamekosana, ukweli uliopo wapenzi hawa wapo pamoja ila ilikua kiki yakuvuta nafsi za watu nakutayarisha njia ya kutangaza ujio wa kibao kipya na cha kwanza kwenye ulingo wa sanaa ya burudani ya muziki cha mrembo na mjasiriamali Vera. Akiongea na meza yetu ya habari ya Dizzim, mtu huyu wa karibu na ambaye hajataka jina lake kutajwa amasema mawazo na uandishi mzima wa wimbo huu kwa jina NALIA, ulifanywa na Otile Brown.

Otile Brown na Vera Sidika

Napia wawili hawa walifahamu fika kuwa walihitaji wafuasi zaidi ndani ya Kenya na Tanzania. Hivyo Otile Brown alikuja na wazo la kumjumlisha rafiki wake wa karibu ambaye pia ni mwanamitindo kutoka nchini Tanzania maarufu kama Kalisa. Kalisa ambaye ndiye aliyetumika kama video model kwenye video ya Nalia yake Vera Sidika inasemekana alilipwa kitita cha haja kupitia mradi huu. Hata hivyo mwanzoni vyombo vingi vya habari za burudani nchini Tanzania, vilikuwa tayari vimeandika habari kuwa Vera ameachana na Otile na kuanza maisha mapya na Kalisa. Uvumi huu ulitokana na kusambaa kwa picha iliyopigwa kwenye nyuma ya pia (Behind the scene) ya video ya Nalia, ilio onyesha Vera akimkabidhi gari aina ya Benz. Huku nyuma sadfa na kukosana kwa Vera na Otile ni kwasababu Otile alimuomba Vera pesa ili kununua gari aina ya Benz. Hatua ambayo ilimfanya mrembo huyo kuanika skirini shoti za mazungumuzo yao ya siri mtandaoni.

Behind the scene video ya Nalia: Mwana Mitindio Kalisa kutoka Tanzania na mrembo Vera Sidika

Hata hivyo kumtumia Kalisa kama model kilkua kitu ambacho kilizua msisimuko mkuu nchini Tanzania, huku wengi wakukubali mbashara kwani wanamfahamu Kalisa kuwa ni bingwa wa mambo yakuwarusha roho wamama na wanadada wengi ndani ya Tanzania. Tayari Kalisa ni baba ya watoto kadhaa aliozaa na wanawake tofauti, na ameshawahi kukiri kwenye vyombo vya habari kuhusu jambao hili. Hivyo wazo hili la kutumika kama video model kwenye video nzima ya Nalia, lilikuwa bora na mwisho wa siku lilitimia huku mbali na kupata ama kuongeza mashabiki ndani na nje ya Africa Mashariki, inasemakana Vera na Otile wameweza kujiingizia kipato cha haja kila mmoja huku Vera akinufaika zaidi kwani bidha zake anazouza zimepata ununuzi zaidi nchini Tanzania kwa kujizolea wateja wapya.

Comments

comments
Share.

About Author

Leave A Reply