Wednesday, August 21

WANAFUNZI WA KIKE WALAZIMISHWA KUVAA KAPTURA

0


Wanafunzi wa kike nchini Uingereza wameanza kulazimishwa kuvaa kaptura au suruali ndani ya sketi zao za shule kutokana na tabia ‘mbaya’ inayofaywa na wanafunzi wa kiume dhidi yao.

Inaelezwa kuwa tabia hii ni ya kuwapiga picha wasichana katika maungo yao ya ndani ya nguo pasipo wenyewe kujua (upskirting), na utaratibu huu mpya unalenga kukomesha tabia hii.

Rais wa Chama cha Waalimu na Wahadhiri (ATL) nchini humo Dr Mary Bousted ameeleza kuwa tabia hiyo ni ya udhalilishaji wa kijinsia kwani baada ya picha hizo kupigwa huwa zinatumwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Tabia hii inaelezwa kukua sana nchini humo na inaendelea kusambaa kutokana na kuongezeka kwa simu za kamera na matumizi ya mitandao ya kijamii baina ya wanafunzi jambo ambalo linafanya wanafunzi wa kike kutokuwa salama.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.