Sunday, August 25

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA WAUMINI KUHUSU KUTOA TAARIFA ZA UNYANYASAJI WA WATOTO KATIKA JAMII.

0


BAADHI YA WATOTO AMBAO NI WAWAKILISHI WA MABARAZA YA WATOTO KUTOKA KATA YA KAHAMA MJINI NA NYANDEKWA WAKIWA KATIKA MAFUNZO HAYO.
KAHAMA
Viongozi wa madhehebu ya dini katika mkoa wa Shinyanga wametakiwa kutoa elimu kwa waumini kuhusu kutoa taarifa za unyanyasaji wa watoto kwa watendaji wa Vijiji na mitaa zinazofanywa na wazazi pamoja na walezi katika jamii zinazowazunguka .

Wito huo umetolewa leo na Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga Bi Grory Mbia katika mafunzo ya siku ya Tatu yanayolenga kuwajengea uwezo kamati za kupinga ukatili wa wanawake na watoto katika halmashauri ya mji wa Kahama.

Mbia amesema Viongozi wa dini wanakutana na watu wengi kwa wakati mmoja hivyo wakitumia nyumba za ibada kuwaelimisha jamii kutoa taarifa za unyanyasaji unaofanyika majumbani itasaidia watendaji wa serikali kufuatilia watu wanaofanya vitendo hivyo katika jamii.

 Kwa upande  wake meneja wa Mradi wa mlinzi wa mtoto haki na utawala kutoka Shirika la RAFIKI SDO ambao ndiyo waandaaji wa mafunzo hayo Shangwe Kimati,amewataka wananchi kuzitambua kamati hizo katika kata zao na kutoa ushirikiano ili kufanikiwa kumaliza unyanyasaji.

Afisa elimu Kata ya Kahama mjini Maria Mpazi ametoa wito kwa wazazi wanaowaficha ndani watoto wenye ulemavu kuwapeleka Shule kwani ni haki yao ya Msingi  huku Imamu wa msikitiki wa Masjid Nuru kata ya Nyandekwa Daud Athuman akiwataka wananchi kuacha kufanya ukatili na badala yake wawe na hofu ya Mungu.

Nao baadhi ya watoto waliopata mafunzo hayo,Wamesema kuwa mafunzo waliyopata yatawasiadia kuwapa elimu watoto wenzao na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya kuwaadhibu watoto bila makosa kwani ndiyo sababu inayopelekea watoto kukimbia majumbani.
Mafunzo ya Siku tatu ya Kuwajengea uwezo Kamati za Kupinga unyanyasaji wa wanawake na watoto yameratibiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la RAFIKI SDO kwa kushirikiana na Halmashauri ya mji wa Kahama  yakiwa na kampeni Isemayo FUNGUKA,Ukatili dhidi ya mtoto Hamuachi mtu salama –Chukua Hatua Mlinde Mtoto.

MATUKIO KATIKA PICHA:
 WAJUMBE WA KAMATI ZA KUPINGA UNYANYASAJI WAKIWA KATIKA SIKU YA PILI YA MAFUNZO KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

  WAJUMBE WA KAMATI ZA KUPINGA UNYANYASAJI KUTOKA KATA ZA KAHAMA MJI NA NYANDEKWA  WAKIWA KATIKA MAFUNZO HAYO.


 MJUMBE WA KAMATI YA KUPINGA UNYANYASAJI MARIAM MASSU AKICHUKUA KUMBUKUMBU ZA YALE WANAYOFUNDISHWA KATIKA MAFUNZO HAYO.

 AFISA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ABUBAKARI KIBAKAYA AKITOA MAFUNZO KWA WAJUMBE WA KAMATI YA KUPINGA UNYANYASAJI KUHUSU HAKI NA WAJIBU WA WAZAZI KATIKA KUMLINDA MTOTO.
 AFISA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ABUBAKARI KIBAKAYA AKIENDELEA KUTOA MAFUNZO.


 BAADHI YA WAJUMBE WAJUMBE WA KAMATI YA KUPINGA UNYANYASAJI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA MAENDELEO WA MKOA HAYUPO PICHANI.

 WAJUMBE WAJUMBE WA KAMATI YA KUPINGA UNYANYASAJI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA MAENDELEO WA MKOA HAYUPO PICHANI.

 AFISA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ABUBAKARI KIBAKAYA AKIWAONYESHA WAJUMBE MFUMO WA USIMAMIZI WA HAKI ZA MTOTO KUPITIA PROJECTOR.

 MAFUNZO YAKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.
 WAJUMBE WAJUMBE WA KAMATI YA KUPINGA UNYANYASAJI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA MAENDELEO WA MKOA HAYUPO PICHANI.

 AFISA MAENDELEO YA JAMII HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA ABUBAKARI KIBAKAYA AKIENDELEA NA MAFUNZO.

WAZEE MAARUFU WA KATA YA KAHAMA MJINI NA NYANDEKWA WAKIWA KATIKA MAFUNZO HAYO.

WAZEE MAARUFU WA KATA YA NYANDEKWA WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAFUNZO YA HAKI ZA WATOTO 
MRATIBU WA MASUALA YA ULINZI WA MTOTO,HAKI NA UTAWALA KUTOKA SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN ALEX ENOCK AKITOA NENO KWA WAJUMBE WALIOHUDHURIA MAFUNZO HAYO.

BAADHI YA WAJUMBE WAKIWEMO VIONGOZI WA DINI WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAFUNZO.
Read More

Share.

About Author

Comments are closed.